Ban ataka kukomeshwa mara moja mauwaji ya waandamanaji wa Syria

Ban ataka kukomeshwa mara moja mauwaji ya waandamanaji wa Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa taarifa kali akiyaalani mauwaji ya wananchi yanayoendelea nchini Syria na kusisitiza kuwa lazima yakomeshwe mara moja.Amezitaka mamlaka za Syria kuheshimu na kulinda uhuru wa wananchi na siyo kuendeleza vitendo vya kuwapinga na kuwasitishia maisha yao.

Ameeleza kuwa mfumo unaoendeshwa na dola kuyadhibiti maandamano hayo ambayo yanayofanywa kwa shabaya kuupinga utawala wa rais Bashar al-Assad ni mfumo unaenda kinyume na  misingi inayozingatia haki za binadamu.Ripoti za hivi karibuni kabisa zinasema kuwa operesheni iliyoendeshwa na vikosi vya serikali kwa ajili ya kuyabana maandamano hayo imegharimu maisha ya raia wasiopungua 1,200 na mamia wengine wakilazimika kuvuka mipaka hadi nchi jirani ikiwemo Uturuki.