Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM uko mbioni kujenga eneo la kumbukumbu ya waathirika wa biashara ya utumwa

UM uko mbioni kujenga eneo la kumbukumbu ya waathirika wa biashara ya utumwa

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mpango wa ujenzi wa pahala ambapo patatumika kama sehemu ya kumbukumbu ya waathirika wa biashara ya utumwa,uko kwenye njia ya kutia matumaini na hii leo kumesainiwa makubaliano maalumu kwa ajili ya kuwakaribisha wazabuni.

Jengo hilo ambalo litatumika kama sehemu ya kumbukumbu ya watu waliopitia mateso ya biashara ya utumwa linatazamiwa kujengwa kandoni mwa yaliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.Kamati inayoratibu ujenzi wa eneo la kumbukumbu leo ilikutana kwa ajili ya kuwekeana saini makubaliano ya kuanza kupokea zabuni juu ya mifumo na michoro ya jengo hilo.Kamati hiyo inaongozwa na uwakilishi toka nchi za Afrika, Jamaica na eneo lote la Caribbean.