Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Oparesheni za kutoa misaada kwenye pembe ya Afrika zatatizwa na ukosefu wa fedha

Oparesheni za kutoa misaada kwenye pembe ya Afrika zatatizwa na ukosefu wa fedha

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo shirika la kilimo na mazao FAO yanatoa wito kwa misaada ya dharura kusaidia hali iliyopo kwenye pembe ya Afrika baada ya eneo hilo kukumbwa na hali mbaya ya ukame.

Mashirika yakiwemo shirika la UNHCR, UNICEF na WFP yanasema yanakabiliwa na upungufu wa fedha kusaidia karibu watu milioni 10 wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula nchini Kenya , Somalia , Ethiopia , Djibout na maeneo ya Uganda. UNHCR inasema kuwa huenda hali ikawa mbaya ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa.Emilia Casella kutoka WFP anasema kuwa bajeti ya shirika hilo ya dola milioni 477 ina upungufu wa dola milioni 190.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)