Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto milioni mbili wakabiliwa na hali mbaya ya utapiamlo:UNICEF

Watoto milioni mbili wakabiliwa na hali mbaya ya utapiamlo:UNICEF

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya watoto milioni mbili kwenye pembe ya Afrika wanakabiliwa na utapiamlo na kwa sasa wanahitaji misaada ya dharura ya chakula kuokoa maisha yao. Kati ya hawa milioni moja kati yao wako kwenye hali inayohatatarisha maisha yao hali ambayo imeathiri kukua kwao kimwili na kiakili.

UNICEF inasema ina mpango ya kuchangisha dola milioni 31 kwa muda wa miezi mitatu ijayo ili kuweza kutoa usaidizi kwa watoto na wanawake wanaokabiliwa na hali mbaya kuwai kulikumba eneo la pembe ya Afrika tangu miaka 50 iliyopita. Marixie Mercado ni kutoka UNICEF.

(SAUTI YA Marixie Mercado)