Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawasafirisha wahamiaji waliokwama nchini Libya

IOM yawasafirisha wahamiaji waliokwama nchini Libya

Mashirika ya kimataifa likiwemo shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na lile la Handcap International yameungana kutoa hamasisho kuhusu hatari inayosababishwa na mabomu yasiyolipuka wakati wa vita. Umoja wa Mataifa na mashirika mengine yasiyokuwa ya kiserikali yamedhibitisha kuwa kuna mabomu na silaha zingine ndogo ndogo kwenye baadhi ya maeneo yenye watu wengi nchini Libya yakiwemo Ajdabiya, Misrata na kwenye milima ya Nafusa.

UNICEF inasema kuwa watoto katika sehemu nyingi nchi libya wako kwenye hatari kubwa na wengine washapoteza maisha yao. Wakati huohuo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeazisha oparesheni za kuwasafirisha kwa njia ya ndege mamia ya wahamiaji kutoka chad waliokwama kwenye mji wa Sebha. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)