Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yazindua mwongozo kuzisaidia nchi zilizokumbwa na mizozo

UM yazindua mwongozo kuzisaidia nchi zilizokumbwa na mizozo

Umoja wa Mataifa umezindua mwongozo maalumu ambao ndani yake kunakutikana miongozo ya kisheria ambayo itatumika kuhamasisha matengamano ya amani katika nchi zilizopitia machafuko ama zile zinazopitia vipindi vya mageuzi.Shabaya kubwa ya mpango huo ni kuzisaidia nchi hizo zinainuka na kuipa utengamano mifumo yake ya kiutawala na kuzifanyia mapitio baadhi ya sera na taasisi zake za kimaamuzi.

Sheria hiyo ambayo imeandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya kitengo kinachohusika na operesheni za ulinzi wa amani na kamishna ya haki za binadamu,inatajwa kama dira ya mwongoza kwa ajili ya kuonyesha viashilio vya mambo.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chombo hicho,Bwana Dmitry Titov ambaye anasimamia vikosi vya ulinzi wa amani, amesema kuwa majaribio ya awali yaliyofanyika nchini Haiti yamedhibitisha namna uwezo wa kufanya kazi kwa mwongozo huo.