Baraza la usalama lafanya marekebisho ili kuwapa fursa zaidi majaji wanaosikiliza kesi za mauwaji ya Rwanda

7 Julai 2011

Baraza la usalama limefanyia marekebisho mfumo uliopo kwenye mahakama inayosikiliza mauji ya kimbari ya Rwanda yaliyofanywa mwaka 1994 ili kutoa nafasi kwa majaji wasiokuwa wa kudumu kwenye mahakama hiyo kuwa na fursa ya kupiga kura kumchagua rais atakayesimamia shughuli za mahakama.

Kwa mujibu wa marekebisho hayo, majaji hao pamoja na sasa kuwa na uwezo wa kupiga kura lakini pia wanaruhusiwa kuwania nafasi hiyo.Baraza hilo limepitisha marekebisho mengine kadhaa ambayo pia yamelenga kutoa nafasi kwa majaji ambao hawajafungamana moja kwa moja kwenye mahakama hiyo kuwa na uwezo wa kuendesha kesi kwa muda wowote watakaohitajika.Rais anayechaguliwa kuongoza jopo la majaji anawajibika kusimamia shughuli zote za mahakama na kutoa usimamizi wa karibu bila kuathiri mwenendo wa uhuru na wajibu wa mahakama hiyo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter