Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rolnik kufanya ziara nchini Algeria

Rolnik kufanya ziara nchini Algeria

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki ya kuwa na makao Raquel Rolnik, anatarajiwa kutembelea Algeria kuanzia tarehe tisa mwezi huu kwa lengo la kuchunguza athari za sera za nyumba za nchi hiyo na mipango ya haki za binadamu kwa watu wake. Rolnik pia atajiribu kuangazia zaidi masuala ya wanawake , wakimbizi wa ndani na wahamiaji.

Ziara hii ya Rolnik inajiri baada ya maandamano nchini Algeria ya kupinga changamoto zilizo katika kupata makao. Baada ya ziara hiyo Rolnik ataandaa ripoti ya mapendekezo jinsi ya kuboresha masuala ya nyumba nchini Algreria ripoti ambayo itawasilishwa mbele ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Machi 2012.