Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumla ya watu milioni 25 wayafanyia kazi makampuni ya ulinzi

Jumla ya watu milioni 25 wayafanyia kazi makampuni ya ulinzi

Ripoti ya mwaka huu ya shirika la Umoja wa Maataifa linalohusika na silaha ndogo ndogo inasema kuwa karibu watu milioni 25 kote dunuani wanayafanyia kazi makampuni ya ulinzi .

Ripoti hiyo inasema kuwa idadi ya kampuni zinazohusiana na ulinzi imeongezeka kwa muda wa miongo mitatu iliyopita. Inasema kuwa makampuni hayo yanamiliki jumla ya bunduki milioni 3.7 ikilinganishwa na bunduki milioni 26 zinazotumiwa na polisi au milioni 200 zilizo mikononi mwa wanajeshi.