Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwimbaji wa Russia atambuliwa na UNESCO

Mwimbaji wa Russia atambuliwa na UNESCO

Mwimbaji mmoja raia wa Russia ametangazwa kuwa msanii mpya ambaye anaingizwa kwenye orodha ya wanamziki waliopewa jukumu la kuwa mabalozi wa hisani wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya elimu sayansi na utamaduni UNESCO.

Moja ya jukumu lake kubwa msanii huyo Alsou Abramova mwenye umri wa miaka 28 ni kuhubiri ujumbe wa amani na upendo.Anatazamiwa kutambuliwa rasmi hapo kesho wakati atapokutana na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova kwenye makao makuu ya shirika hilo Mjini Paris.  Kuchaguliwa kwake kunakuja na mchango wake mkubwa wa kuyasaidia makundi ya watu walioko pembezoni.