Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waipongeza India namna inavyokabiliana na maambukizi ya HIV

UM waipongeza India namna inavyokabiliana na maambukizi ya HIV

Umoja wa Mataifa umepongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na serikali ya India namna inavyokabiliana na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya HIV.Kulingana na shirika hilo la Umoja wa Mataifa linalohusika na mapambano dhidi ya ugonjwa huo UNAIDS, India imepiga hatua kubwa kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo kupitia mipango yake ikiwemo ile inayolenga kukabiliana na maambukizi mapya.

India inatajwa kufanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi mapya kwa zaidi ya silimia 50 katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita. Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel Sidibé amesifu juhudi hizo na kuongeza kuwa India inatemebea kwenye ramani ya matumaini