Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu ni moja ya haki za binadamu na ni lazima ilindwe : Singh

Elimu ni moja ya haki za binadamu na ni lazima ilindwe : Singh

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kupata elimu Kishore Singh amewataka viongozi wa dunia kukubali kuwa elimu ni haki muhimu ya kibinadamu ambayo inastahili kulindwa kutokana na ugumu wa kiuchumi. Akiongea kwenye mkutano wa kila mwaka wa baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC mjini Geneva Kishore Singh amezishauri nchi kuhakikisha kuwa zimefadhili ipasavyo sekta ya elimu.

Kulingana na takwimu za sasa ni kuwa watoto milioni 67 kote duniani hawaendi shuleni huku wale wanaofanikiwa kwenda shuleni mara nyingi wakipata viwango vya chini vya elimu . Singh amesema kuwa bajeti za kitaifa ni lazima zitengewe  fedha zaidi kwa sekta ya elimu akiongeza kuwa ni jambo la kusikitisha wakati matumizi ya kijeshi yanakuwa zaidi kushinda matumuzi ya elimu.