Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna uwajibikaji na haki kwa waathiriwa wa ubakaji DRC: UM

Hakuna uwajibikaji na haki kwa waathiriwa wa ubakaji DRC: UM

Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu uliotekelezwa katika eneo la Walikale jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo zaidi ya watu 387 walibakwa kati ya tarehe 30 na tarehe 2 mwezi Agosti unaonyesha kuwepo ukosefu wa uwajibikaji , haki na usalama kwa waathiriwa .

Ripoti kutoka ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kuhusu ubakaji na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliangazia uovu uliotekelezwa kwenye vijiji 13 ambapo mamia ya watu walibakwa wengine 116 kutekwa na zaidi ya nyumba kuteketezwa. Ripoti hiyo pia inasema kuwa kati ya watu 387 waliobakwa 300 walikuwa ni wanawake , wanaume 23, wasichana 55 na watoto wavulana 9.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)