Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

De Schutter kufanya ziara ya kwanza nchini Afrika Kusini

De Schutter kufanya ziara ya kwanza nchini Afrika Kusini

Mjumbe maalum wa Umoja wa Maataifa anayehusika na masuala ya haki ya kuwa na chakula Olivier De Schutter atafanya ziara rasmi nchini Afrika Kusini kuanzia tarehe 7 hadi 15 mwezi huu ili kuweza kufahamu hatua zilizochukuliwa na serikali katika kutekeleza haki ya kupata chakula.

Kulingana na takwimu za hivi majuzi karibu asilimia 14 ya wananchi wa Afrika Kusini hawana usalama wa chakula huku asilimia 25 ya watoto walio chini ya miaka 6 wakishindwa kukua. Afrika Kusini imekuwa kwenye mstari wa mbele katika kuunga mkono haki ya kuwa na chakula na hata kuijumuisha kwenye katiba yake lakini hata hivyo Bwana De Schutter anasema kuwa bado kuna changamoto kadha. Ziara hiyo inalengo la kukagua jinsi Afrika kusini inavyolinda haki ya kuwa na chakula na jitihada inazofanya katika kutatua changamoto zilizosalia.