Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atia uzito mchakato unaofanywa na Ugiriki ili kufanikisha misaada wa kiutu huko Gaza

Ban atia uzito mchakato unaofanywa na Ugiriki ili kufanikisha misaada wa kiutu huko Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameongeza uzito kuunga mkono hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali ya Ugiriki inayoendesha jitihada za kutumia magari yake ya ndani kusafirisha misaada ya kibinadamu kuwafikia mamia ya wananchi walioko ukanda wa Gaza.

Hatua inafanywa kwa kuzingatia pia mashauriano ya karibu na Umoja wa Mataifa.Ugiriki imeonyesha utayari wake kuendelea kutumia njia zilizoko nchini humo ili kufikisha misaada hiyo.Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Waziri wa mambo ya Nje wa Ugiriki Stavros Lambrinidis, Ban amesema kuwa uamuzi huo utatazamiwa kupunguza hali ya wasiwasi juu ya kukwama mpango wa upelekaji wa misaada kwenye eneo hilo.

Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa imeweka shabaya ya kuendelea kufanya kazi kwa karibu na mamlaka za Ugiriki, Israel na Palestina ili kuondosha kizingiti kilichowekwa na Israel ambacho kinakwaza juhudi za upelekaji misaada kwenye eneo hilo.