Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFAD yataka uwekezaji kwenye kilimo ili kukabili janga la njaa Afrika Mashariki

IFAD yataka uwekezaji kwenye kilimo ili kukabili janga la njaa Afrika Mashariki

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mpango wa maendeleo ya kilimo IFAD limeonya  juu ya tabia ya kupuuzia mambo na kutaka kuchukuliwa kwa hatua za haraka ili kuzia uwezekano wa kutokea janga la mkwamo wa ukosefu wa chakula katika eneo la afrika mashariki.

Ripoti zinasema kuwa zaidi ya watu milioni 10 kwenye eneo hilo kwa hivi sasa wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula na kunauwezekano kuwa hali hiyo inaweza ikapindukia zaidi katika siku za usoni.

Bwana Geoffrey Livingstone ambaye ni wanauchumi wa shirika hilo amesema kuwa kuna haja ya kuwepo kwa uwekezaji makini katika sekta hiyo ya  kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula.Katika taarifa yake mtaalamu huyo amesisitiza kuwa hakuna njia nyingine ya mkato  itayoweza kuliokoa eneo hilo la balaa la njaa kama kutakosekana uwekezaji kwenye kilimo na kuwapa zingatio wakulima wa kima cha chini.