Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna uhaba wa madawa nchini Libya: WHO

Kuna uhaba wa madawa nchini Libya: WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa taifa la Libya kwa sasa linakabiliwa na uhaba wa madawa na bidhaa zingine za kutoa huduma za matibabu . WHO inasema kuwa inafanya mazungumzo na kamati ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu vikwazo kuweza kutumia pesa za serikali ya Libya katikza kununua madawa. Tarik Jasarevic kutoka WHO anasema kuwa uhaba huo wa madawa unashuhudiwa kwenye maeneo yanayodhibitiwa na serikali na pia waasi.

(SAUTI YA TARIK JASAREVIC)

WHO pia inasema kuwa upungufu unaweza kudhoofisha uwezo wa watoto huduma za kiafya katika kuwahudumia majeruhi wa vita  na watoto.