Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la haki za binadamu kutoka UM linalozuru Yemen layatembelea maeneo kadha

Kundi la haki za binadamu kutoka UM linalozuru Yemen layatembelea maeneo kadha

Kundi la haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa linalozuru Yemen limekutana na makamau wa rais wa nchi hiyo, viongozi wa upinzani, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na waandamanaji kwenye miji ya Sanaa na Taiz.

Kundi hilo limeendesha mahojiano na kuzuru maeneo mawili ya mji wa sanaa ambapo waandamanaji wanaoipinga serikali wamekuwa wakikusanyika. Kundi hilo pia limejionea hali ilivyo kwenye mji wa Taiz na pia kuzuru sehemu iliyoshambuliwa Mei 29 kabla ya kuzuru hospitali mbili zilizoporwa.

Rupert Colville msemaji wa ofisi ya UM ya haki za binadamu anasema kuwa kundi hilo limeruhusiwa kuingia mji ya Sanaa na Taize na kufahamishwa kuhusu mipanago ya serikali ya kuanzisha mazungumzo kuhusu mabadiliko ya kisiasa.