Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wimbi jipya la mabadiliko katika nchi za Kiarabu ni ishara ya hitajio la haki za binadamu kwa kila mtu-Pillay

Wimbi jipya la mabadiliko katika nchi za Kiarabu ni ishara ya hitajio la haki za binadamu kwa kila mtu-Pillay

Afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki binadamu ameelezea wimbi la mageuzi linaloendelea kuvuma katika nchi za kiarabu na maeneo ya Kaskazini mwa bara la afrika ni ishara kwamba usawa wa haki za binadamu ni kilio cha kila mtu tena katika wakati wote. Kamishna huyo wa haki za binadamu Navi Pillay,amesema kuwa mkusanyiko wa matukio yanayojiri huko Afrika ya Kaskazini  na katika eneo la mashariki ya kati linaarifu namna shabaya iliyomo kwenye tamko la kimataifa juu ya kuzingatiwa kwa haki za binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Geneva, Pillay amefahamisha kuwa katika kufikia shabaya ya kuwa na usawa wa haki za binadamu hakuna mipaka tena ya kusema kwamba sehemu hii inapaswa itendewe hivi na sehemu ile itendewe vile, bali binadamu yote wanayo haki ya kufikiwa na haki za binadamu.Ameeleza kuwa matukio yaliyojiri nchini Tunisia na Misri yametoa ukweli wa mambo namna miiko na viambaza vinavyokwaza haki za binadamu vinavyoweza kuondolewa kwa nguvu ya umma.