Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuongezeka kwa wakimbizi Kenya kunazidisha hali ya wasiwasi zaidi-UM

Kuongezeka kwa wakimbizi Kenya kunazidisha hali ya wasiwasi zaidi-UM

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya usamaria mwema limearifu hali ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la wakimbizi wanaowasili nchini Kenya wakitokea eneo la Pembe ya Afrika jambo ambalo linazua kitisho kingine kwenye eneo  hilo.

Kwa mujibu wa shirika hilo OCHA, idadi kubwa ya wakimbizi imeendelea kumiminika katika kambi ya Dadaab na kufanya eneo hilo kuanza kuzidiwa na idadi ya wakimbizi, kitendo ambacho imeonya kuwa inaweza kuzusha mkwamo mwingine kwa kimazingira.

Kambi hiyo iliyoko Kaskazini  Mashariki mwa Kenya hadi sasa inaarifiwa kuwa na jumla ya wakimbizi 353,921 ikiwa ongezeko la zaidi ya mara nne ya uwezo wake.Hali hiyo inafanya kambi hiyo iwe ndiyo kubwa zaidi duniani kwa huhifadhi wakimbizi kwa wakati mmoja.