UNHCR yalalamikia kuuawa kwa watu wawili kwenye kambi ya Dadaab

1 Julai 2011

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa takriban watu wawili wameuawa na wengine kadha kujeruhiwa katika eneo la Dagahley kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya kufuatia maandamano wakati polisi walipojaribu kutawanya umati uliokuwa ukipinga ubomoaji makao yaliyojengwa kiharamu kwenye kambi hiyo.

Tangu mwanzo wa mwaka huu zaidi ya wakimbizi 61,000 wametafuta hifadhi nchini Kenya hali ambayo imesababisha kuwepo kwa msongamano mkubwa kwenye kambi. Kambi ya Dadaab kwa sasa ina wakimbizi zaidi ya 370,000. Immanuel Nyabera msemaji wa UNHCR nchini Kenya amezungumza na idhaa hii.

(SAUTI YA IMMANUEL NYABERA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud