Mamia ya wanawake nchini DRC wabakwa.

1 Julai 2011

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeripoti kuwa takriban wanawake 121 wamebakwa na wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwenye mkoa wa Kivu kusini mwezi Juni mwaka huu. Kisa hicho kimeripotiwa kufanyika kati ya tarehe 11 na 12 mwezi Juni kwenye kiji cha Nyakiele kilicho mbali mkoani Kivu Kusini.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliozuru eneo hilo juma moja lililopita umesema kuwa wakati wa shambulizi hilo wanajeshi pia walipora mali na kutekeleza vitendo vingine katili kwa wenyeji wa kijiji hicho. Rupert Colville ni kutoka ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa ni lazima uchunguzi ufanyika ili kuwafikisha mbele ya sheria wahusika.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud