Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuendelea kulisaidia bara la Afrika kuwawezesha vijana:Migiro

UM kuendelea kulisaidia bara la Afrika kuwawezesha vijana:Migiro

Umoja wa Mataifa umesema utaendelea kulisaidia bara la Afrika kutimiza malengo ya kulijenga vyema taifa la kesho ambalo ni vijana.

Kauli hiyo imetolewa mbele ya wakuu wan chi na serikali za Umoja wa Afrika wanaokutana mjini Malabo Equatorial Guinea kwa mkutano wa sikuu mbili unaomalizika Julai Mosi .

Mada kuu ya mkutano imekuwa ni kuwawezesha vijana kwa ajili ya maendeleo stahimilivu au endelevu, lakini suala la Libya na mengine ya amani na usalama yamechukua nafasi kubwa katika mkutano huo.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro ndiye aliyebeba bendera ya Umoja wa Mataifa na ujumbe maalumu unaojumisha nia ya Umoja wa Mataifa kuendelea kuisaidia Sudan Kusini, kusaidia juhudi za Umoja wa Afrika kupata sluhisho nchini Libya, lakini kubwa zaidi ni ujumbe wa kuwawezesha vijana wa Afrika kama alivyomweleza mkuu wa Idhaa hii Flora Nducha.

(MAHOJIANOYA FLORA NA ASHA ROSE MIGIRO)