Watoto wa Gaza waweka rekodi kwenye mashindano ya msimu wa joto

30 Juni 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limesema kuwa zaidi ya wanafunzi 3000 kwenye ukanda wa Gaza hii leo wameweka rekodi mpya kati ya rekodi nne wanazonuia kuvunja msimu huu wa joto kwa kurusha miavuli mingi kwa pamoja hewani.

Margot Ellis naibu kamishna mkuu kwenye shirika la UNRWA amesema kuwa takriban watoto 3,500 kutoka Gaza walirusha miavuli 176 baada ya kuijaza hewa na kupaa juu ya uwanja wa Khan Younis kwenye tamasha linalotajwa na UNRWA kuwa la kuangazia jamii ya maelfu ya watoto waliofungiwa. Naye msemaji wa UNRWA Chris Gunners anasema kuwa ikiwa watoto katika ukanda wa Gaza watapatiwa nusu ya fursa ya kuwa huru kutoka kizuizi wataonyesha uwezo wao na kuwa namba moja duniani.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter