Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka wanaowashambulia watoto kwenye mizozo kuchukuliwa hatua

Ban ataka wanaowashambulia watoto kwenye mizozo kuchukuliwa hatua

Akiongea kwenye mkutano ulioandaliwa na mjumbe maalum wa masuala ya watoto na mizozo Radhika Coomaraswamy pamoja na balozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa Peter Wittig, Ban amesema kuwa kando na kutaja na kuaibisha pia wana njia  watakayotumia kulinda shule na hospitali zilizo kwenye maeneo ya mizozo. Ban ameongeza kuwa kulinda shule na hospitali ni wajibu wa Umoja wa Mataifa sawia na kuwalinda watoto kutoka kwa wanaowanyima haki za elimu na huduma za kiafya.