Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM utaendelea kushirikina na viongozi wa Afrika kuhakikisha kuwa uchaguzi ni njia ya kuleta amani:MIGIRO

UM utaendelea kushirikina na viongozi wa Afrika kuhakikisha kuwa uchaguzi ni njia ya kuleta amani:MIGIRO

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana kwa karibu na viongozi wa kiafrika katika kujenga na kudumisha amani ili kuhakikisha kuwa uchaguzi ni mwelekeo wa kuleta amani na wala si ghasia.

Migiro ameyasema hayo hii leo akihutubia mkutano wa 17 wa muungano wa Afrika unaofanyika Malabo nchini Equatorial Guinea, ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono jitihada za waafrika za kupata haki ya kuchagua viongozi wao. Mada kuu katika mkutano huo ni kuwazesha vijana na kuchagiza maendeleo endelevu na huo ndilo ujumbe ambao bi Migiro ameufikisha kwenye mkutano huo kutoka kwenye Umoja wa Mataifa.

(SAUTI ASHA ROSE MIGIRO)

Mkutano hu wa siku mbili ulioanza leo na ambao una masuala ya vijana utajadili changamoto zingine zinazoikabili Afrika na utamalizika kesho ijumaa.