Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya kuchunguza mauaji ya Rafik Hariri yatangaza waranti wa kukamatwa

Mahakama ya kuchunguza mauaji ya Rafik Hariri yatangaza waranti wa kukamatwa

Mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri imetangaza waranti nne kwa watu wanaoshukiwa kuhusika kwenye mauaji hayo. Ripoti zinasema kuwa waranti hizo zinawalenga maafisa wa ngazi za juu kutoka kundi la Shia na kutoka lile la Hezbollah.

Hariri na watu wengine 22 waliuawa mwezi Februari mwaka 2005 mjini Beirut wakati kulipotea mlipuko mkubwa wa bomu msafara wake ulipokuwa ukipita. Waranti hizo zimezua maoni tofauti nchini Lebabon huku wengi wakitaka kujua nani alimuua Hariri.

Lakini hata hivyo miaka mingi ya kusubiri kesi hiyo imesababisha watu wengi kuwa na shaka ikiwa ukweli utabainika. Awali mkuu wa mashtaka nchini Lebanon alithibitisha kuwa alipokea waranti za kukamatwa kwa watu wanne kutoka kwenye mahakama hiyo