Ban atoa wito kwa nchi kuchukua hatua zaidi kuwaingiza wanawake zaidi bungeni

30 Juni 2011

 

 

 

 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa ni nchi chache ambazo zimefikia lengo la kuingiza asilimia 30 ya wanawake bungeni . Akiongea kwenye mkutano unaojadili njia za kuwashirikisha wanawake kwenye demokrasia Ban amesema kuwa hatua zinastahili kuchukuliwa ili kuupunguza pengo lililopo.

 

Ban amesema kuwa masuala ya uwajibikaji na uwazi yanapatikana tu kwa njia ya sheria , sera na hatua maalumu zinazo shughulikia masuala ya kutokuwa na usawa. Amesema kuwa ikiwa wanawake watatengwa demokrasia zitakuwa hatarini. Hata hivyo Ban amewashukuru wanawake kwa jitihada wanazochukua wao wenyewe katika kupata nafasi za juu kwenye serikali na kuongeza usawa unaanza wakati mtoto wa kike anapata haki ya chakula , afya na elimu sawa na mtoto wa kiume

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter