Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazitaka nchi za Ulaya na Asia ya Kati kuachana kuwapeleka watoto kwenye vituo vya kulelea

UM wazitaka nchi za Ulaya na Asia ya Kati kuachana kuwapeleka watoto kwenye vituo vya kulelea

 

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamezitolea mwito nchi za Ulaya na Asia ya Kati kuachana na mwenendo wake wa kuwahifadhi watoto kwenye maeneo inayotumia kuwatunzia watu wasiojiweza kwani uzoefu unaonyesha kuwa mwenendo kama huo unazua kitisho cha ustawi kwa watoto wengi.

Kulingana na shirika la  Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na ile kamishna ya haki za binadamu, zaidi ya watoto milioni pamoja na watu wazima wanaolelewa kwenye vituo maalumu wanaendelea kusalia kwenye maeneo hayo na baadaye kupotea kabisa. Mashirika hayo mawili yameanzisha kampeni inayotaka kuachwa kwa tabia hiyo hasa kufutia ripoti kadhaa zilizotolewa hivi karibuni ambazo zinaelezea ustawi mbaya wanaokumbana nao watoto kwenye makambi hayo.

Serikali nyingi barani Ulaya na sehemu ya Asia hutumia mfumo wa kuwawekwa kwenye makambi maalumu watoto wenye ulemavu lakini wakosoaji wanasema kuwa hatua hiyo inawanyima fursa ya kujiendeleza na kukosa ustawi bora.