Skip to main content

UNESCO yapongeza kuachiwa kwa waandishi wa Kifaransa huko Afghanstan

UNESCO yapongeza kuachiwa kwa waandishi wa Kifaransa huko Afghanstan

Ripota Hervé Ghesquière na mpigapicha wake Stéphane Taponier,ambao wanafanya kazi katika kituo cha France 3 Television walitekwa nyara sambamba na mkalimani wao Reza Din wakati wakiendelea na uandaaji wa makala katika eneo la mashariki mwa Afghanistan.

Hata hivyo wote watatu pamoja na watu wengine wawili imeelezwa wameachiwa huru leo.  Katika taarifa yake UNESCO imesema imepokea kwa furaha kubwa habari za kuachiwa huru kwa waandishi hao na ikawapongeza wale wote waliofanikisha mpango huo.