Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama laongeza muda wa MUNUSCO DR Congo

Baraza la usalama laongeza muda wa MUNUSCO DR Congo

 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongezea muda wa mwaka mmoja kwa vikosi vya kulinda amani kuendelea kusalia nchini Congo. Kwa maana hiyo vikosi hivyo vitasalia nchini humo hadi June 30, mwaka ujao wa 2012.

Azimio la kuongeza muda huo lilipitishwa kwa kishindo katika upigaji kura uliofanyika kwenye kikao chake New York.

Kupitia azimio hilo, baraza hilo la usalama limedhibitisha shabaya yake ya kuendelea kutoa ulinzi wa raia pamoja na mali zake hasa katika maeneo yaliyokumbwa na mkwamo wa amani.

Kikosi hicho kinachoijulikama kama(MONUSCO) kina jumla ya watumishi wanaofikia20,000 ambao wamegawika kulingana na asili ya majukumu yao.