Skip to main content

Wapalestina wataka UM kulitambua taifa lao

Wapalestina wataka UM kulitambua taifa lao

Viongozi wa kipalestina wanaokutana mjini Brussels kwenye mkutano wa amani ya mashariki ya kati wanautaka Umoja wa Mataifa kulitalitambua taifa hilo.

Mazungumzo kati ya Wapalestina na Waisrael yamekwama tangu mwaka uliopita baaada ya Israel kukataa kusitisha ujenzi wa makaazi ya walaowezi wa kiyahudi kwenye ardhi iliyotwaliwa ya Wapalestina.

Mkutano huo wa kimataifa wa siku mbili wa Umoja wa Mataifa unaunga mkono mpango wa amani kati ya Isreal na Palestina unaotafuta njia mbadala ya kufanyika kwa mazungumzo ikiwemo kupatikana kwa mataifa mawili.