Wataalamu wa mazingira wazitaka nchi kuanzisha nishati mbadala

29 Juni 2011

Kamati ya wataalamu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ikijishughulisha na masuala ya tabia nchi IPCC imeyataka mataifa duniani kuwajibika kupunguza utoaji wa gesi chafu kwa madai kuwa kwa kufanya hivyo kutaleta ustawi mkubwa kwenye maeneo ya usalama wa nishati, afya, na ukuzaji wa ajira.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Rajendra Pachauri amesema kuwa wakati umefika kwa serikali kuanza kutekeleza shabaya ya upunguzaji wa matumizi teknolojia zinazoharibu mazingira na badala yake kuanzisha mipango mipya ambayo ameita kuwa ni rafiki na yenye tija kubwa.

Kulinga na ripoti iliyoanishwa na kamati hiyo, ulimwengu unaweza kufikia shabaya ya kuzalisha nishati kwa zaidi ya asilimia 80 ifikapo mwaka 2050 kama itaweka mbadala wa matumizi wa teknolojia rafiki kama Sola.Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza haja ya kuanzisha matumizi ya nishati mbadala akisema kuwa ulimwengu hauwezi kukwepa hatua hiyo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter