Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuendelea kuwepo kwa MONUSCO nchini DRC ni muhimu kwa wanawake wa nchi hiyo: Wallstrom

Kuendelea kuwepo kwa MONUSCO nchini DRC ni muhimu kwa wanawake wa nchi hiyo: Wallstrom

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya ukatili wa kimapenzi kwenye mizozo Margot Wallstrom amekaribisha uamuzi wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wa kuongeza muda wa kuhudumu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wa MONUSCO.

Muda wa kuhudumu wa Monusco umeongezwa kwa mwaka mmoja zaidi huku kikosi cha kulinda amani cha MONUSCO kikitarajiwa kuhudumu nchini humo hadi Juni 30 mwaka 2012. Wallstrom amesema kuwa ni muhimu kuwa muda huo umeongezwa kwa kuwa bado kuna changamoto za kiusalama nchini DRC akiongeza kuwa visa vya ubakaji kwenye eneo la Fizi , kusinu mwa Kivu ni ishara kuwa wanawake nchini DRC bado wako kwenye hatari.