Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya kimataifa ya maji yavutia ahadi za kufadhili miradi ya maji kwenye jimbo la Darfur

Kamati ya kimataifa ya maji yavutia ahadi za kufadhili miradi ya maji kwenye jimbo la Darfur

Serikali ya Sudan , wafadhili pamoja na mashirika mengine wameonyesha nia ya kutoa ahadi kutokana na wito wa kiamataifa uliozinduliwa kwenye mkutano wa maji wa kimataifa wa Jimbo la Darfur uliondaliwa mjini Khartoum kati ya tarehe 27 na 28 mwezi huu.Umoja wa Mataifa na wizara ya unyunyizaji na raslimali ya maji nchini Sudan walitoa wito wa dola bilioni moja fedha zitakazofadhili miradi 65 ya maji ili kuleta suhulu la uhaba wa maji kwenye jimbo la Darfur na katika kusuluhisha moja ya sababu za mzozo unaondelea.

Zaidi ya wataalamu 500 wa maji , halmashauri , wataalamu wakiufundi na waakilishi wa mashirika ya kimataifa walishiriki kwenye mkutano huo. Emmanuel Mollel ni mkuu wa mradi wa maji na mazingira wa mpango wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur UNAMID na anafafanua kuhusu ahadi na fedha za kusaidia mradi huo

(SAUTI EMMANUEL MOLLEL)