Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhaba mkubwa wa chakula washuhudiwa kwenye pembe ya Afrika:WFP

Uhaba mkubwa wa chakula washuhudiwa kwenye pembe ya Afrika:WFP

Mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Josette Sheeran amesema kuwa hali ya ukosefu mkubwa wa chakula inayoshuhudiwa kwenye pembe ya Afrika imehataraisha maisha ya mamilioni ya watu ambao tayari wanakabiliana na kupanda kwa bei ya chakula na mizozo. Karibu watu milioni 9 wengi wakiwa akina mama na watoto kwa sasa wanahitahi misaada ya kibinadamu nchini Somalia , Ethiopia , Djibouti , Kenya na sehemu fulani nchini Uganda.

WFP ina lengo la kuwalisha zaidi ya watu milioni 6 wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. Sheeran anasema kuwa WFP itachukua hatua za haraka kukabiliana na janga hili linalosababisha wakulima kuuza mali yao hasa vifaa vya kilimo na mifugo ambavyo ni tegemeo lao la kimaisha.