Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majanga yasiyotabiriwa ni hatari kwa uchumi wa nchi za Asia – Pacific

Majanga yasiyotabiriwa ni hatari kwa uchumi wa nchi za Asia – Pacific

Umoja wa Mataifa umesema kuwa kuendelea kushuhudiwa kwa hali mbaya ya hewa pamoja na majanga yasiyotabiriwa ni kati ya masuala ambayo yamerudisha nyumba kukua kwa uchumi na maendeleo kwenye nchi za Asia- Pacific hali amabayo inahitaji kuwepo kwa ushirikiano.

Katibu kwenye tume ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa kwenye nchi za Asia - Pacific Nagesh Kumar anasema kuwa eneo la Asia- Pacific linajaribu kujikwamua kutoka kwenye hali mbaya ya kiuchumi na majanga mengine ya kiasili masuala ambayo yamekwamisha jitihada za eneo hilo katika kutimiza malengo ya milenia.