Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM barani Afrika aweka zingatio la vijana

Afisa wa UM barani Afrika aweka zingatio la vijana

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa barani Afrika ametoa mwito wa kutaka kuyawezesha zaidi makundi ya vijana yaliyomo barani humo wakisema kuwa matukio ya hivi karibuni yaliyojiri kwenye maeneo ya Afrika ya Kaskazini yamesabibisha kwa kiwango kikubwa vijana hao wasali bila kazi.

Amesema kuwa matukio hayo yanawaacha vijana wengi wakiwa kwenye njia panda wengi wao wakiendelea kulalamikia uhuru na usawa huku wengine wakipigania haki za msingi na mageuzi ya kweli.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Afrika Katibu Mkuu wa Kamishna inayohusika na masuala ya uchumi kwa Afrika Abdoulie Janneh, amesema kuwa vijana wa leo ndio wanaoshikilia hatma ya ulimwengu wa sasa.Ametaka kufanyika kwa uhamasisho wa dhati kwa vijana wa afrika ili wafikiwe vyema na ujumbe unaohubiri maendeleo endelevu kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadaye.