Bodi ya IMF yamteua Christine Lagard kuwa mkurugenzi mkuu mpya wa IMF

28 Juni 2011

Bodi kuu ya shirika la fedha duniani (IMF) hii leo imemteua Christine Lagarde kuchukua wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa IMF na pia mwenyekiti mwandamizi wa bodi kuu kwa kipinndi cha miaka mitano kitakachoanza tarehe tano mwezi Julai mwaka huu.

Bi Lagarde anayechukua mahala pa Dominique Strauss-Kahn ni mwanamke wa kwanza kuchukua wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa IMF tangu kubuniwa kwa shirika hilo mwaka 1944.

Bi Lagard ameteuliwa na bodi ya wanachama 24 wanaowakilisha nchi 187 wanachama wa IMF na kumaliza mpango uliowekwa na bodi kuu wa kufanya uteuzi huo.

Bi Lagarde mwenye umri wa miaka 55 aliye na shahada ya unasheria ashahudumu kama waziri wa fedha na pia kama waziri wa biashara nchini ufaransa mwaka 2007

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter