Maeneo mengine nane yaingizwa kwenye historia ya urithi wa dunia

28 Juni 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu,sayansi na utamaduni UNESCO limetangaza kuongeza maeneo mengine nane katika orodha ya sehemu zinakutikana urithi wa dunia.Kwa mujibu wa UNESCO maeneo hayo yaliyotambuliwa sasa ni kutoka barani Afrika,Ulaya, Mashariki ya Kati na Asia.

Miongoni mwao kunakutikana Fort Jesus iliyoko nchini Kenya na eneo moja linapatikana nchini Ethiopia linalojulikana kama Konso.Kamati ya kuhifadhi utamaduni wa kale ambayo inaendelea na kikao chake cha 35 inasema kuwa hadi sasa inaendelea kuchunguza maeneo mengine yapatayo 35 kabla ya kuyatangaza kama yanafaa kuingizwa kwenye urithi wa dunia.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter