Ugonjwa wa Sotoka watokomezwa duniani. Shukrani kwa juhudi za kimataifa:FAO

28 Juni 2011

Mkutano wa Shirika la Kilimo na Mazao la Umoja wa Mataifa FAO umetangaza rasmi kuangamizwa kwa ugonjwa unaoathiri mifugo wa Sotoka kote duniani. Ugonjwa wa Sotoka umewaua mamilioni ya ngombe , Nyati na wanyama wengine na kuchangia kuwepo kwa njaa na kuzorota kwa uchumi barani Afrika , Asia na Ulaya.

Kwenye azimio lake mkutano huo umetoa wito kwa jamii ya kimataifa kufuatilia kwa makini na kuhakikisha kuwa virusi na chanjo za ugonjwa huo vimehifadhiwa kwa njia inayofaa kwenye mahabara na utafiti kuhusu ugonjwa huo kufanywa. Tangazo hilo ni hatua ya mwisho kwenye kampeni ambayo imechukua miongo kadha ya kuuangamiza ugonjwa wa Sotoka.Madibo Traore ni mkurugenzi msaidizi wa kilimo wa FAO.

(SAUTI YA MADIBO TRAORE)