Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamilioni ya watu wakabiliwa na uhaba wa chakula kwenye Pembe ya Afrika:UM

Mamilioni ya watu wakabiliwa na uhaba wa chakula kwenye Pembe ya Afrika:UM

Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu milioni 10 kwenye eneo la upembe wa Afrika wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kwa sasa wanaihitaji misaada ya chakula ya kuokoa maisha. Nchi tano kwenye eneo hilo zikiwemo Djibouti, Ethiopia, Kenya Somalia na Uganda kwa sasa zinakabiliwa na hali mbaya ya kiangazi kuwahi kushuhudiwa kwa muda wa miaka 60 iliyopita.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa utapia mlo miongoni mwa watoto kwenye maeneo hayo umeongezeka mara dufu huku mizozo ikisababisha idadi kubwa ya Wasomali kukimbilia kambi nchini Kenya na Ethiopia. Elizabeth Byrs kutoka shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA anasema kuwa uwezo wa familia kuishi kulingana na hali hiyo umedhoofishwa na kupanda kwa bei ya chakula.