Ocampo ataoa sababu ya kutangazwa waranti wa kukamatwa kwa rais wa Libya na watu wengine wawili

28 Juni 2011

Mwendesha mashtaka kwenye mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC , Luis Moreno-Ocampo amesema kuwa mahakama hiyo ilitangaza kukamatwa kwa rais wa Libya muammar Gadaffi, mwanae na afisa mmoja wa serikali kwa kuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliomba hatua kuchukuliwa.

Ocampo amesema kuwa watatu hao watakamatwa kwa kuwapiga risasi raia kwenye mitaa na kwa kuwaua wapinzani wao wakiwa nyumbani mwao. Ocampo amesema kuwa lazima watatu hao wakamatwe na utawala wa Libya hata kama taifa la Libya si mwanachama wa mahakama ya ICC lakini kwa misingi kuwa Libya ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter