Mkuu wa UNICEF aanza ziara ya siku tatu nchini Kyrgyzstan

28 Juni 2011

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kuwahudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Anthony Lake yuko kwenye ziara ya siku tatu nchini Kyrgyzstan kushuhudia hatua zilizopigwa kuwasaidia watoto baada ya nchi hiyo kushuhudiwa mzozo wa kisiasa mwaka mmoja uliopita.

Kwenye ziara yake Lake atafanya mkutano na rais Roza Otunbayeva, waziri mkuu Almazbek Atambayev , Spika wa bunge, wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Bwana Lake pia atatembelea eneo la Osh kusini mwa Kyrgyzstan na kufungua kituo cha vijana kwenye kijiji cha Asanchek na baadaye kukutana na washirika wa UNICEF kwenye jumba wanamozalia akina mama la Kara Suu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter