Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tawala dhalimu zitawajibishwa-Pillay

Tawala dhalimu zitawajibishwa-Pillay

Tawala zinazoendesha mamlaka zake kimabavu na kidikteta pamoja na maafisa wengine wanaojifunganisha na mienendo hiyo wametahadharishwa juu ya uwezekano wa kutumbukizwa kwenye sheria za kimataifa.

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu Navi Pillay amesema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka waathirika wa mateso, ambayo yameadhimishwa June 26.

Bi Pillay ameonya kuwa tawala za aina yoyote zinazokumbatia matukio ya aina hiyo kamwe haziwezi kukwepa kuwajibika mbele ya sheria za kimataifa na kuongeza kuwa uwepo wa mahakama ya uhalifu dhidi ya binadamu ni mfano unaojitosheleza .