Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jose Graziano da Silva kutoka Brazil ndio mkurugenzi wa FAO

Jose Graziano da Silva kutoka Brazil ndio mkurugenzi wa FAO

Graziano da Silva mwenye umri wa miaka 61 kutoka nchini Brazili amechaguliwa kuwa mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la chakla na kilimo la Umoja wa mataifa FAO baada ya kupata kura 92 kati ya 180 na kumshinda mpinzani wake Miguel Moratinos Cuyaube waziri wa mambo ya nje wa Hispania aliyepata kura 88.

Uchaguzi huo umefanyika katika siku ya pili ya mkutano wa FAO wa mwaka unaohudhuriwa na wajumbe wote wanachama ambao utapiga kura pia kupitisha bajeti ya shirika hilo kwa mwaka 2012 hadi 2013.

Alipokuwa waziri wa usalama wa chakula na kupambana na njaa nchini Brazili bwana Da Silva aliwajibika na kutekeleza mpango uliofanikiwa wa serikali wa kuhakikisha kuna njaa sufuri . Mpango huo ulisaidia kuwatoa watu milioni 24 kwenye umasikini uliokithiri na kupunguza utapia mlo nchini Brazili kwa asilimia 25 katika kipindi cha miaka mitano.

Na tangu mwaka 2006 amekuwa mkurgenzi mkuu msaidizi na mwakilishi wa FAO wa kanda ya Amerika Kusini na Caribbean. Baada ya kushinda alikuwa na haya ya kusema.

(SAUTI YA GRAZIANO DA SILVA)

Da Silva alizaliwa Novemba 17 mwaka 1949 na ana elimu ya Udaktari wa udhamili katika masomo ya sayansi ya uchumi, lakini stashahada na shada za masuala ya kilimo, sociolojia na uchumi vijijini. Anakuwa ni mkurugenzi mkuu wa nane tangu kuanzishwa kwa FAO 16 Oktoba mjini Quebec Canada mwaka 1946. Da Silva anayezungumza Kiingereza, Kispanish na Kireno anachukua nafasi ya Jaques Diouf kutoka Senegal na ataanza kazi rasmi Januari mosi 2012 hadi Julai 31 mwaka 2015.