Juhudi za kimataifa zimezinduliwa kukabili tatizo la maji na vita Darfur

27 Juni 2011

Umoja wa Mataifa na wizara ya umwagiliaji na mali ya asili ya maji ya Sudan leo wamezindua ombi maalumu la kukabiliana na ongezeko la kasi la kupungua kwa rasilimali ya maji Darfur. Kwa kufanya hivyo watakuwa wanatatua moja ya sababu kubwa za mgogoro unaoendelea wa Darfur na kuchangia kuleta msingi imara wa amani ya kudumu.

Akielezea tatizo la maji ambalo linawaathiri watu wote wa Darfur na hasa wasiojiweza Profesa Ibrahim Gambari mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika UNAMID amesema athari za upungufu wa maji zitakuwa kikwazi katika juhudi za kufikia amani ya kudumu na utulivu kwenye jimbo la Darfur. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter