Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kupunguza mipango ya msaada wa chakula Afghanistan

WFP kupunguza mipango ya msaada wa chakula Afghanistan

Mamilioni ya Waafghanistan huenda wakakosa msaada wa chakula baada ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP kupunguza msaada wake kutokana na upungufu wa fedha unaokabili shirika hilo.

WFP inasema ufadhili uliopatikana unatosheleza tu kuwasaidia watu milioni 3.8 nchini Afghanistan kati ya idadi ya awali ambayo ni milioni 7.3 wanaohitaji msaada wa chakula. Shirika hilo linasema linahitaji fedha zaidi ambazo ni dola milioni 220 mwaka huu ili kuendelea na kazi yake Afghanistan kama ilivyopangwa hapo awali.

Miongoni mwa mipango ambayo itabidi ipunguzwe ni programu za kulisha mashuleni ambazo WFP inasema zimekuwa muhimu sana katika kuinua kiwango cha uandikishaji watoto shuleni. Challiss McDonough ni msemaji wa WFP nchini Afghanistan.

(SAUTI YA CHALLIS McDONOUGH)

WFP inasema takribani nusu ya wilaya zote 34 za Afghanistan zitaathirika na kupunguzwa kwa msaada huo wa chakula.