Walioshitakiwa kwa uharamia Mombasa wawasilisha malalamiko mahakama kuu Kenya

24 Juni 2011

Wanaume 24 raia wa Somalia walioshtakiwa wiki hii katika mahakama ya Mombasa nchini Kenya kwa madai ya kuhusika na uharamia, sasa wamewasilisha ombi katika mahakama kuu wakilalamikia jeshi la Denmark.

Kupitia mawakili wao Justus Munyithya na Gerald Magolo wanasema wanajeshi wa Denmark waliwatesa na kuwajeruhi, kando na kuwazuilia kwa kipindi kirefu kinyime cha sheria.

Washukiwa hao wameshtakiwa kwa madai ya kuiteka nyara meli ya uvuvi iitwayo ARIYA katika bahari iliyo ghuba ya Oman mwezi Oktoba mwaka jana, wakijihami kwa silaha hatari kama vile bunduki aina ya AK 47. Umoja wa Mataifa umekuwa msitari wa mbele kupiga vita masuala ya uharamia kwenye Pwani ya Somalia.

 Mwandishi wa habari Josephat Kioko alikuwa mahakamani Mombasa, kufuatilia kesi hiyo ya uharamia, na kuandaa taarifa hii.

(PKG NA JOSEPHAT KIOKO)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter