Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kukusanya takwimu za raia wa Guinea Bissau wanaoishi uhamishoni

IOM kukusanya takwimu za raia wa Guinea Bissau wanaoishi uhamishoni

Ikijibu ombi la Guinea Bissau, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limeanza kukusanya taarifa za raia wa nchi hiyo walioko huko Ureno na Ufaransa katika kile kinachoelezwa kuwa kufanikisha kongamano kubwa liliko usoni.

 Baadaye mwaka huu wananchi wa Guinea waliko barani Ulaya wanatazamiwa kuwa na kongamano ambalo litajishughulisha zaidi ya masuala ya maendeleo.

 Hata hivyo Guinea-Bissau inakabiliwa na tatizo la kukosekana kwa wataalmu wa kutosha, kwani idadi kubwa huelekea katika nchi za Ulaya kwa ajili ya kusaka ajira.  Takwimu kutoka serikali zinaonyesha kwamba zaidi ya raia 40,000 wanaishi nchini Ureno wakati wengine 20,000 wapo ufaransa.